The Earth’s breath, by Ben Munyao [a reblog]

MZUNGUKO WA DUNIA Dunia yangu, dunia yetu,inapumua kwa uchungu,ikilia kimya chini ya jua kali,ikimeza moshi, majivu na machozi.Misitu inang’olewa,miti inakatwa,matawi yanalia kwa upepo,majani yanatamani mvua. Mvua ilichelewa,mvua ikawa haba,mto ukakonda,mashamba yakanyamaza,na mbegu zikabaki zikingojabusu la maji angani. Joto limejaa juu ya paa,joto limejaa jangwani,joto limeingia majumbani,na watoto wanauliza:“Kesho itakuwa na kivuli?” Bahari inapanda,kingo zinatetemeka,mawimbi yanameza […]

Leave a comment